





Chercher à obtenir l’interview du chef Maï-Maï Jackson, c’est comme piocher dans le dernier carré de ceux qui se nomment Vraix Patriotes, Résistants, ou Défenseurs du territoire Congolais mais dont la vie tient sur un petit fil même s’ils tutoient la mort.
Ce chef Maï-Maï a, malgré-lui, accepté de répondre à mes questions tout en sachant qu’il est recherché par la Mission des Nations Unies au Congo (Monuc) et le Gouvernement Congolais. Il serait accusé de semer des troubles dans le territoire de Rutshuru, lui qui se dit combattre les "Banyarwanda" et tout autre "traître" oeuvrant pour la colonisation de l’Est du Congo par des pays étrangers.
Jackson qualifie les autorités militaires de Goma de "Complices de Paul Kagame et du RCD". Il dénonce la partialité dans le processus de l’unification des armées. Il se pose la question de savoir ce que ses troupes iraient faire dans les camps que les rwandophones désertent pour rejoindre Laurent Nkunda? Jackson se gausse des grades militaires et autres avantages accordés aux Mai-Maï à Kinshasa et il redoute les troubles qui perturberaient les prochaines élections générales dans le Grand-Nord.
Toute cette introduction est le résumé de l’interview qu’il m’a accordée en Kiswahili mais dont le poids de ses mots et l’intensité de sa voix peuvent ne pas se ressentir sur le web.
Benilubero.com: Bwana Jackson hujambo? Ni kwa sababu gani wewe waendelea kupigana huko sehemu za Goma na ijapo vita ime malizika Kongo?
Jackson: Kongo vita haiya isha kwani wanyarwanda hawajarudi kwao. Wakingali naendelea na ideologia na mipango yao mbali-mbali kwa kuiba mali ya Kongo na kuwa uwa wa Kongomani.
Benilubero.com: Ni nani mkubwa wenu?
Jackson: Ni sisi wenyewe tunaji shiriki kwa kupigania haki yetu. Hakuna mtu anaweza kuitika baba, mama na ndugu wauawe na asiwapiganiye.
Benilubero.com: Umetafutwa na serikali ya Kinshasa pia na Monuc hata wame kugonga toka Rutshuru, wakikushika utauawa ama utatiwa gerezani?
Jackson: Hiyo si neno la kushangaza. Monuc haiwezi kutowa maadui mahali walipo. Wa kina Gemadari Laurent Nkunda wapo na Monuc inajua mahali walipo. Monuc ikinitafuta ama serikali ya Kongo ni kwa sababu wanataka niache kupigania uma. Inaonekana kama Monuc inafanya ubaguzi kwa kusaidia wale maadui.
Benilubero.com: Sasa ni wewe adui ya Monuc ama Monuc ndiyo adui wako kwani umejificha leo?
Jackson: Sivyo. Tumewasiliana na Monuc.Hawaelewi fikra yangu. Nimewaeleza wanisaidiye tu pige adui alakini inaonekana kama wana mipango mingine, wanishike kusiwe tena mutu wakupigania raiya. Tumewasiliana na Monuc, na mkuu wao gemadari SADI hapo NYAMILIMA. Nimewasiliana na tumekuwa na mazungumuzo na wakuu wa kijeshi kama akina gemaradi MBUYI. Nili wafafanulia ya kwamba mimi sipigani na wa Kongomani ila na pinza hawa majambazi ambao wamevuka mipaka hadi huku kutuvamia. Na kabla hawajarudi Rwanda, mimi sita acha mapambano hata kamwe.
Benilubero.com: Ukitaja raiya, unamaanisha nini?
Jackson: Tazama, huko sehemu za Rutshuru raiya wa Kongo wanahamishwa ukimbizini juu ya adui na Monuc inajua mahali alipo Laurent Nkunda.
Benilubero.com: Ni hakikisheni ya kwamba wewe na kina Nkunda, Kakolele pia wenginewo ni kama maadui wa Monuc na serikali ya Kongo?
Jackson: Mimi sina shida na serikali ya Kongo hata na Monuc.
Benilubero.com: Umeanzisha mapigano na adui toka mwaka gani na ulikuwa wapi?
Jackson: Tangu zamani nimepinzana na hawo wavamizi wa inchi yetu. Toka utawala wa Mobutu na hata tangu miaka sitini na tatu. Mimi nilikuwa vichakani, na leo pia niko vichakani.
Benilubero.com: Ni nani toka Kinshasa anakupa vikosi na mshaada?
Jackson: Mimi sina usaidizi wa watu wa siasa toka Kinshasa. Serikali ya Kinshasa ina tumika na yule gemadari wa Goma"Tango-Fort". Huyu mtu ni msaliti. Huyu mtu anafanya siasa ya Paul Kagame, anapokea watu na vikosi toka Rwanda na mimi sisikii kwa nini serikali ya Kinshasa inaaminia yule gemadari"Tango-Fort"ijapo ni mtumishi wa Rwanda, ni msaliti.
Benilubero.com: Hayo mambo unaaminisha ni usaliti wa taifa!
Jackson: Unajuwa ya kwamba mbele ya muungano wa taifa na ugenzi wa serikali ya 1+4 kila watu walikuwa na kundi lao la mapigano. Wengi hawajafunguwa siri zao. Huyo "Tango-Fort"alikuwa wa chama cha RCD-Goma na leo ana sema uwongo anatumika na serikali alakini mimi najuwa ya kwamba yeye ni mtumwa wa KAGAME. Kwa mfano mapambano ya mji wa Nyamilima, watu wake"Tango- Fort"wakina Colonel AMISI na wa luteni FRANCOIS, wa kina ZAIRE na major MAKENGA walitumikisha vikosi kutoka Rwanda.
mbele ya muungano wa taifa na ugenzi wa serikali ya 1+4 kila watu walikuwa na kundi lao la mapigano. Wengi hawajafunguwa siri zao. Huyo "Tango-Fort"alikuwa wa chama cha RCD-Goma na leo ana sema uwongo anatumika na serikali alakini mimi najuwa ya kwamba yeye ni mtumwa wa KAGAME.Kwa mfano mapambano ya mji wa Nyamilima, watu wake"Tango- Fort"wakina Colonel AMISI na wa luteni FRANCOIS,wa kina ZAIRE na major MAKENGA walitumikisha vikosi kutoka Rwanda.
Benilubero.com: Kwa nini huwezi kutoa hizo siri zote ukiwa ndani ya majeshi ya Kongo,mbali na vichaka ulimo leo?
Jackson: Majeshi ya Kongo,hata yamechangwa hayana nguvu moja.Kuna wengine ambao wana neon la kusema na wengine ni wakutimiza tu.Askari walio toka kwa kundi la RCD wanakuwa kama ndio wa kuu,wana vyeo vya kuongoza watakavyo.Hiyo "Intégration"siya kawaida.
Benilubero.com: Sasa utafanya vita hadi uchaguzi? Kunabaki kama miezi mine tu raiya apige kura!
Jackson: Mimi si amini kama uchaguzi utakuwa na hali shwari sehemu za huko Rutshuru. Vijiji vingi vimeunguzwa na adui, wakaaji wametiwa ukimbizini, hata raiya wamekata tamaa. Kumepita juma mbili tu huko KATUGURU na ngambo za ISHASHA nyumba samanini na mbili zimeunguzwa na adui. Hawo ndugu wanao teswa na kulala inje porini, uniambieni wata kuja siku gani kwa uchaguzi?
Benilubero.com: Ni askari wangapi unao katika jeshi lako kwa kupigana na Laurent Nkunda?
Jackson: Mimi nina vikosi vya kutosha.
Benilubero.com: Wakakuita Kinshasa wakupe cheo ama pesa utatamani uwe gemadari kwa jeshi, muheshimiwa kwa bunge ama nani?
Jackson: Sipiganiye cheo, sipiganiye franga, sipigane kwa umimi. Na pigania raiya. Uma ikapata usalama, mabeberu wakatoka inchini, wasaliti wakaacha mambo mapoovu, ndiyo itakuwa mafanikio kwangu. Mbona watu wengine wamepata vyeo, wengine wamepata pesa Kinshasa, kumekuwa makundi na makundi ya wa Maï-Maï, na amani haija rudi inchini. Kwa nini hao ma gemadari, watu wa bunge na wengine wote hawalete amani Kongo?
Benilubero.com: Asante sana Bwana Jackson.
Jackson: Sawa Bwana.
Mazungumuzo pamoja na Mai-Mai Jackson yamerikodiwa tarehe 27-februari-2006 na Magloire Paluku kwa niaba ya Beni-Lubero Online.





